0715 72 92 92

SHABAN KALUSE

Kwa Matangazo na mambo mbalimbali & Wasiliana Nami

http://www.serenahotels.com/serenadaressalaam/default-en.html

Jun 14, 2016

Mwanamke Unaweza kuwa mtabiri jinsi mwenzi wako atakavyokuwa baada ya miaka kumi……


[​IMG]

Ndio kwanza mmeanza uhusiano ambapo mnaelekea kufunga ndoa, wote bado ni vijana wabichi, hamna majukumu makubwa yanayohitaji fedha, hamna watoto, kwa hiyo fedha mnazopata ni kwa ajili ya kula na kusogeza maisha kidogo, huku mkipanga mipango yenu ya baadae kuhusu kufunga ndoa. Katika kipindi hiki kila mmoja anajaribu kuishi kama malaika, hataki kumkwaza mwenzake. Hata kama mwenzake amemkosea atakaa kimya na kuumia ndani kwa ndani kwa sababu ya hofu ya kuogopa kuonyesha tabia zake pale akasirikapo.

Tabia hiyo huwapa wakati mgumu wapenzi kujuana tabia, hususan kwa wanawake ambao hutamani sana kuwajua wapenzi wao jambo ambalo huwawia vigumu kutokana na sababu nilizozieleza hapo juu. Lakini zipo tabia ambazo anaweza kuwa nazo mwanaume ambazo ki ukweli hazina maana yoyote kwa wakati huo lakini zinakupa ujumbe mahsusi kwamba huko mbeleni mwanaume huyo uliye naye atakuwa mume mwema au hatakuwa mali kitu zaidi ya kuwa sawa na mzigo usiyo na mwenyewe.

Hapa chini nitaeleza baadhi ya vijitabia ambavyo vitakufanya umjue mwanaume uliye naye kama atakuwa ni mume wa namna gani:

1.Je huwa anazungumza na watu wazima wanaomzidi umri?

Wakati mnapokuwa mmehudhuria hafla yoyote ambayo inajumuisha watu wa rika mbalimbali, Je mwanaume uliye naye huwa anazungumza na vijana wa rika lake au chini ya rika lake au anajichanganya na watu wazima waliomzidi umri? Kwa kawaida mwanaume kijana ambaye mara jingi katika mjumuiko wa marika mbalimbali huwa anazungumza na vijana wa rika lake au chini ya rika lake anadhihirisha kwamba huyo bado hajakua na hayuko tayari kujifunza kutoka kwa watu waliyomzidi umri. Lakini mwanaume kijana anayependa kujumuika na watu wazima waliyomzidi umri ambaye anapenda kusikiliza mazungumzo kuhusu maisha yao ya mahusiano na mafanikio yao katika maisha ni ishara kwamba anataka kujifunza na kukua. Hapo ni kama anatafuta maarifa ya kuingia katika maisha ya baadaye. Pamoja na hayo pia awe na tabia ya kutopenda kwenda kwenye nyumba za starehe usiku na kujumuika na vijana wenzie na kunywa pombe usiku kucha. Na kama ni mitoko iwe ni ile ya staha na mapema awe amerudi nyumbani kwake. Kijana huyu awe na tabia ya kujifunza kutoka kwa watu mbalimbali na pia ajenge mahusiano na watu waliofanikiwa. Hii ni dalili nzuri kwamba anafaa kuwa mume.

2.Je huwa anakuficha kuhusu mambo yake?

Je huwa anakushirikisha kuhusu madhila yake yanayomletea msongo wa mawazo? Je huwa anakupigia kukujulisha kuhusu mazonge yaliyomkuta akiwa kwenye shughuli zake? Kama anakushirikisha hii ni dalili kwamba ni mtu wa kujali familia. Ni mtu anayemthamini mwenzi wake na anayependa kumshirikisha mwenzi wake kwenye mambo yanayomletea msongo wa mawazo. Lakini kama ni mtu ambaye anaficha hisia zake chungu na hapendi kumshirikisha mwenzi wake kwenye mambo yanayomletea msongo wa mawazo zaidi ya kupendelea kuwa naye wakati wa siku za furaha, huyo haonyeshi kuwa mume mwema mbeleni kwani kushirikishana katika hisia ziwe ni chungu au za furaha ni msingi wa kujenga mahusiano imara.

3. Anakuwa na tabia gani baada ya kurudi kazini?

Je yeye ni mtu wa kukimbilia remote na kuwasha TV na kisha kukaa kitako na kuangalia huku akiwa na kinywaji chake baridi alichochukua kwenye jokofu? Je ni mtu ambaye mawazo yake yametawaliwa na kazi au shughuli anazozifanya? Yaani yeye akirudi badala ya kuzungumza na wewe kuhusu siku yako ilivyokwenda badala yake anazungumzia kazi zake au shughuli zake kisha anakaa kimya.

Mwanaume, anayejali zaidi kazi yake au mambo yake au hobby zake hawezi kuwa mume bora na mwenye kujali familia huko mbeleni. Je atawezaje kujali watoto? Je atawezaje kufuatilia maendeleo ya watoto shuleni? Je atawezaje kujua hali ya mwenzake kwa muda ambao hawakuwa pamoja. Dalili hiyo inaonyesha hali ya choyo na ubinafsi na bila shaka kama awali anakuwa na mwenendo huo basi huko mbeleni hali inaweza kuwa mbaya zaidi.

4.Je ni mtu wa kutapanya pesa au kuweka akiba?

Je bwanako ni mtu wa kujirusha na starehe na mwenye matumizi yasiyo na tija? Kama ni ndivyo alivyo, Je huwa anajuta kwa matumizi aliyoyafanya? Kama ni mtu wa matumizi, je huwa anapofanya hivyo huwa anahisi kushtakiwa na dhamira?  Ukweli ni kwamba kuna aina mbili za watu wenye tabia ya matumizi yasiyo ya lazima. Kuna wale ambao hujihisi kutawaliwa na matumizi yasiyo ya lazima wanajua kwamba wanatumia fedha zao vibaya lakini hawana uwezo wa kujiondoa katika hali hiyo na mara nyingi ni watu wa majuto. Aina ya pili ni ya watu wanaotumia fedha zao bila kujali lakini wanajiamini kwamba hawatapata matatizo ya kifedha yaani wana uhakika wa kipato chao. Huyu wa pili hana matatizo kwa sababu ana uhakika wa kipato na matumizi yake ana uhakika hayataathiri akiba yake aliyojiwekea huyu utakuwa na uhakika wa kuwa salama kwa sababu anajua kuishi kulingana na kipato chake yaani anatumia lakini ana uhakika kwamba kipato kipo na akihitaji fedha hapepesi macho maana zipo tofauti na yule wa kwanza ambaye ni mtu wa matumizi yasiyo ya lazima wakati kipato chake hakina uhakika ni cha kugongea ulimbo. Huyu anaweza kukuweka roho juu wakati wowote.

5.Je ni mtu wa kupanga mipango na kuisimamia au wa kungoja kuongozwa?

Je mwanaume uliye naye ni mtu wa kujichanganya na na makundi ya watu na kuwa mtu wa kutoa mawazo mbalimbali kiasi cha kufanywa kiongozi kwa kuaminiwa au ni mtu wa kusubiri kupangiwa na kuongozwa kila mahali? Mwanaume yeyote mwenye kutangulizwa mbele katika jambo lolote anafaa kuwa si kiongozi tu katika maeneo yake ya kazi bali pia hata katika familia. Lakini yule anayeongozwa kuanzia kazini kwake na hata katika vikundi vidogo vidogo vya mtaani huyo atakuwa na shida kidogo katika kuongoza familia yake. Ni kwamba kuwa na mwanaume wa aina hiyo atakupa wakati mgumu pale ambapo litajitokeza jambo ambalo litahitaji usimamizi wake au kuingiza familia katika kufikia malengo fulani.

6.Je ni mtu anayejali afya yake?

Je huwa ana kawaida ya kufanya uchunguzi wa afya yake mara kwa mara ili kujihakikishia usalama wake kiafya? Je ni mtu wa kufanya mazoezi madogo madogo hata kama anakuwa amebanwa na shughuli zake?  Je huwa anakula vyakula kiafya, yaani siyo mtu wa KUBUKANYA? Je ni mvutaji wa Sigara? Vipi kuhusu matumizi ya dawa za kulevya au bangi? Je ni mtu ambaye anatumia kilevi kistaarabu kama ni mnywaji, au ni mtu wa kukesha kwenye vilabu akilewa bila mpangilio? Kwa kawaida mtu yeyote anayejali afya yake ina maana kwamba anajua thamani ya mwili wake kwamba ndiyo unaomfanya yeye aishi kwani mwili huu wa nyama ndiyo unaobeba uhai wetu kama ukiona mtu anaufuja mwili wake bila kujali kwa ina maana hajui thamani ya yeye kuishi hapa duniani. Mwanamke tafadhali kuwa makini na mwanaume asiyejali afya ya mwili wake. Mwanaume asiyejali afya ya mwili wake ni wazi atakuwa hana malengo katika maisha yek kwani kwa kawaida mtu mwenye malengo anajua thamani ya kulinda afya ya mwili wake kwa sababu anajua wazi kwamba malengo bila afya imara ni kazi bure!

7.Je Marafiki zake ni wa namna gani?

Je marafiki zake ni watu wa kuaminika? Au ana kundi la marafiki ambao wanafanana mawazo na humfanya awe na furaha wakati wote? Lakini ukweli ni kwamba atika maisha yetu huwa tunaathiriwa na watu wanaotuzunguka. Kwa hiyo kama marafiki wa mwenzi wako ni wa rila la kwenye miaka ya 30 hivi na kama bado anaishi ghetto na rafiki au marafiki zake na bado ni watu wa kujirusha labda pamoja na kuvuta bangi na kukesha kwenye vilabu vya usiku. Hii siyoa ishara nzuri na inakupa taarifa kwamab huyu mwanaume bado hajajiandaa kubeba majukumu ya kifamilia. Lakini kama ameshatoka kwenye makundi hayo na akawa anaishi kwenye chumba chake pake yake na kutumia muda wake mwingi kwa mambo yanayohusu taaluma yake na kushiriki na marafiki waaminifu lakini kwa kiasi huku akiweka uzingativu kwenye malengo yake, huyo bila shaka atakuwa ni mume mwema.

8.Je huwa anajisikiaje kuhusu wazazi wake?

Kama wazazi wake wana uwezo, Je huwa anajisikia na kuringia uwezo wa wazazi wake kiasi kwamba haonyeshi dalili za kujitafutia maisha yake mwenyewe? Je ni mtu wa kutegemea kila kitu asaidiwe na wazazi wake au ni mtu wa kupambana na maisha kivyakevyake na kama ni kusaidiwe kuje baadaye? Je ni mtu mwenye kuvutiwa na juhudi za wazazi wake na kutaka kuwa kama wao kwa juhudi zake mwenyewe? Lakini vipi kama wazazi wake ni masikini, Je ni mtu wa kuonyesha kuchukia umasikini wa wazazi wake kiasi cha kujitoa ili kupambana na maisha ili kuepuka yale maisha waliyopitia wazazi wake? Je ni mtu wa kuwasaidia wazazi wake kwa hali na mali? Majibu ya maswali hayo yatakupa picha kwamba mwenzi uliye naye ni mtu wa namna

9.Je ni mtu wa kusongeka mara kwa mara?

Mtu wa kusongeka (Stressers) mara kwa mara  hawezi kujificha, utamjua pale atakapopata changamoto za maisha ambazo siyo za kuumiza kichwa kivile. Na kama hujamjua mwenzi wako kama ni mtu wa kusongeka jaribu kusubiri hadi pale atakapopata changamoto ambayo ni ya kawaida ambayo si ya kuumiza kichwa halafu angalia namna atakavyoipokea.

Je ni mtu wa kutoa msaada hata bila kuombwa?

Kwa mfano kama kuna rafiki yake anahama. Je ni mtu wa kujitolea kumsaidia kuhama au mpaka aombwe? Je na kama ni mtu mzito katika kutoa msaada kwa watu wake wa karibu labdea mpaka aombwe, Je maamuzi yake ni ya namna gani, anakubali moja kwa moja au ni mtu wa kutoa visingizio au hata kama anakubali lakini haishi kulalamika awapo mbali na rafiki huyo? Wapo baadhi ya wanaume si wepesi wa kukubali kutoa msaada hapo kwa hapo mpaka wakajishauri ndipo hukubali, hao hawana matatizo lakini je hata baada ya kukubali huwa ni mlalamishi?

No comments:
Andika Maoni Maoni

This Blog Designed by DonSoo, Contact 0656212326.DonSoo
Kaa Karibu na Mimi